Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

SIKU 2 YA 8

Kumfikiria mwingine.

Ukarimu ni kuwafikiria wengine ambako huturuhusu sisi kumkaribisha Mungu katika hali yake,, tukionyesha upendo wetu kwa wengine. Watu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu, wakiwa na mahitaji yale yale ya kibinadamu. Tunapowaendea wengine kwa huruma na uwazi kusikiliza uzoefu wao, tutaweza kuelewa vizuri mahitaji yao.

Mgeni anaweza kuwasili akiwa amechoka, ana njaa au wakati mwingine ameumia. Kuwapumzisha kwa chakula na pumziko ni wajibu. Tunaona jibu la Ibrahimu kwa wageni wasiojulikana katika Mwanzo 18 na majibu ya Msamaria Mwema kwa mgeni aliyejeruhiwa katika mfano wa Yesu aliowashirikisha wanafunzi wake katika Luka 10. Kukaribisha na kujibu mahitaji ya wengine ni agizo maalum kutoka kwa Mungu na maelekezo aliyoyafanya Yesu kwa uwazi sana kwa wanafunzi wake wa kwanza (Mathayo 10:40-42).

Kwa utendaji, kutoa ukarimu sio kila wakati itakuwa rahisi. Lakini kama wafuasi wa Yesu, lazima tuinuke juu ya magumu yanayokabiliwa. Tunaweza tukawa wazito kufungua milango yetu na kuwakaribisha ndani wale ambao wametusababishia maumivu na kutukatisha tamaa. Wakati kusambaza ukarimu kunaonekana kuwa kugumu, tunaweza kumwita Mungu atusaidie tutimize wajibu huu, badala ya kusita kwetu abadilishe na kutupa uhakika na kuamua kwa huruma. Katika hali yetu, watu wa Kongo wana ukarimu sana sio tu kuhusu watu wa rika yao bali pia kwa wale walio maskini au wasiojiweza na kwa wageni.

Ukarimu ni tabia inayotufundisha namna ya kufungua mioyo yetu kwa wengine bila ya manung’uniko au malalamiko, kuwapokea kwa kuwajali, kuwasikiliza na kutoa malazi na chakula bila malipo.

Tunapoweka kikomo cha ukarimu wetu, tunajinyima sisi wenyewe furaha ya Mungu.

Kwa ajili ya kutafakari:

Niko tayari kiasi gani kuufungua moyo wangu kwa wengine na kuwapa ukarimu kwa uhuru?

Maombi kwa ajili ya leo:

Mpendwa Baba wa Mbinguni, amsha moyo wangu kwa upendo wako ili niweze kuwakaribisha wengine katika maisha yangu, popote ninapoweza kuwa na yeyote ninayeweza kukutana naye leo. Amina.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.

More

Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipango inayo husiana