Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

SIKU 6 YA 8

Kumkumbatia kila mmoja.

Kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu, utamaduni wa kushirikiana kikombe cha chai ni muhimu. Nyakati hizi hutupa muda wa kupumzika, kushiriki na kupata kufahamiana. Kuchukua muda wa kufurahia chai pamoja hutengeneza nafasi ya kushirikiana. Baadaye katika kifungu hiki cha Biblia, Yesu anaomba kukaa chini mezani na Zakayo. Watu katika upana wa hadithi wakajiuliza kwanini Yesu atoe ombi kama hili. Zakayo hakuwa chaguo la kila mmoja la kuwa mwenzi kwenye ‘chai’.

Watu wanaoishi na ulemavu wakati mwingine hujikuta wanaachwa wanywe chai peke yao. Rafiki yangu aligundua kwamba baada ya ibada ya Jeshi la Wokovu, watu hawakuchagua kukaa kunywa chai ya asubuhi mezani na dada yake. Dada yake wa thamani aliishi na ulemavu na hakuwa mwepesi kuelewa kila mara. Ingawa dada huyu hakutengwa kunywa chai ya asubuhi – uwepo wake kwa kweli haukukubalika. Mwana theolojia, John Swinton, anatukumbusha kwamba, ‘Yesu alikaa na watu wale ambao jamii haikutaka kukaa nao.’[1]

Kuchagua nani tunakaa naye hutoa mawasiliano kwa mtu huyo na kwa dunia pana kwamba tunashukuru kwa uwepo wake na uzoefu wake wa dunia. Ukarimu mwaminifu unakubali kwamba watu wa pande zote wanaokaa kuzunguka birika la chai hudhihirisha sura ya Mungu na kuwa na karama za kushirikishana na kila mmoja. Kuchagua kukaa na mtu anayeonekana kuwa tofauti na sisi ni alama ya msingi ya mfumo wa ukarimu wa Kristo.

Kwa ajili ya kutafakari:

Unapofikiria kuhusu hali yako, ni watu gani ambao Yesu anaweza kuwa anakutaka unywe chai nao leo?

Ni kwa njia zipi utafuatilia ukarimu mwaminifu na watu wenye ulemavu katika jamii yako?

Maombi kwa ajili ya siku ya leo:

Baba, tusaidie tuone sura ya Mungu ikidhihirishwa katika kila sura tunayokutana nayo. Tuongoze twende zaidi ya maneno ya kukaribisha na tuelekee kwenye ukarimu unaotafuta kujenga mahusiano. Amina.

[1]John Swinton, “Using Our Bodies Faithfully: Christian Friendship and the Life of Worship,” Journal of Disability & Religion 19 (2015): 239.

Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.

More

Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org

Mipango inayo husiana