Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano
Kukubalika.
Ukarimu wa Kikristo huenda zaidi ya ishara rahisi za wema; huwakilisha kukubalika kimsingi kwa wengine, bila kujali historia yao, imani, au mazingira. Kukubalika hakutegemei ni kiasi gani au ni upungufu kiasi gani tunafahamu kuhusu mtu aliye mbele yetu.
Moja ya maelekezo yanayofahamika sana ya kuonyesha ukarimu yanapatikana katika Agano Jipya kitabu cha Waebrania: ‘ Msisahau kuwafadhili wageni, maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua’ (Waebrania 13:2). Maelekezo haya sio yasiyo na msingi.
Katika Mwanzo 18, tunasoma kuhusu ukarimu mnyenyekevu wa Ibrahimu kwa wageni watatu. Ibrahimu mtu tajiri na mwenye umri, angeweza kumwita mmoja wa watumishi wake wengi awahudumie wageni hawa watatu ambao walikuwa hawafahamiki. Bali Ibrahimu kwa ukarimu aliwapa vile vizuri sana alivyokuwa navyo. Kuna mengi sana ambayo hatuyajui kuhusu wageni hawa. Ibrahimu na Sara nao hawakuwafahamu wao ni akina nani. Lakini mwitikio wao ulikuwa mwitikio wa kuwakubali kimsingi. Na, kama ilivyokuja kuonekana, walikuwa wamemkaribisha Bwana na malaika wawili.
Tunapo wakaribisha wageni, wale ambao hatuwafahamu, tunaweza bila kukusudia tukakaribisha uwepo wa mbinguni katikati yetu – ni ya ajabu namna gani!
Katika Luka 10, tunakutana na mfano wa Msamaria Mwema. Mfano huu unaonyesha jibu la kibinadamu la Msamaria kwa mgeni aliyeumizwa, jibu ambalo linapita mipaka ya kikabila na kidini.
Msamaria hakusimama akajiuliza kama huyu mgeni aliyeumizwa alikuwa ni jirani yake kabla hajamwonyesha upendo; hakufikiria ni wa taifa gani, kabila, hali, au ni msafi. Alikuwa jirani na hilo lilitosha.
Ukarimu wa kweli hauna mipaka na una utayari wa kuwakubali hata wale wanaoonekana kuwa watu wa nje. Hawapo watu wa nje kwenye upendo wa Mungu. Na hakuna sifa inayohitajika ili kupokea au kutoa ukarimu.
Kwa ajili ya kutafakari:
Je, wewe hupalilia roho ya ukarimu inayotoa sura ya kukubalika bila masharti iliyoonyeshwa na Kristo?
Maombi kwa ajili ya leo:
Twaomba Bwana atupe neema ili tuendeleze ukarimu ulio ndani ya kukubalika kwa dhati, tukifuata mfano wa Kristo, aliyewakaribisha wote kwa upendo na huruma. Amina.
Kuhusu Mpango huu
Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.
More
Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org