Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Fungua Milango. Fungua Mioyo.Mfano

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

SIKU 1 YA 8

Usumbufu.

Mwanamke alikuja kuabudu. Kihalisia alikuwa amepinda kiunoni. Hawezi kusimama wima. Macho yake yalikuwa kwa kudumu chini na yamekuwa hivyo kwa karibu maisha yake yote. Kama mwanamke katika jamii hii, yeye ni kipande cha mali isiyo na uwezo. Kama mwanamke aliyelemazwa na roho mwovu – amekwisha kutangazwa ana dhambi naye ni tishio kwa jamii ya dini...na bado, anakuja kuabudu. Bado hajaiacha imani yake au Mungu wake.

Yesu anamwona naye anasema – ‘Tazama mwanamke.’

Tazama: Zingatia! Uwe makini!

Kwa miaka 18, watu wamemuepuka kama tauni – kwa macho yao na mguso wao – na bado, Yesu anamwona, na anamleta katikati ya jamii ya imani; anazungumza naye na kumkusanya katika kumbatio la uponyaji la Mungu. Akarejeshwa.

Yesu anapomwita ‘Binti wa Ibrahimu’, anampa heshima, utu na nafasi katika jamii. Ilikasirisha namna gani!

Ukarimu (siku ya Sabato!) na matokeo ya muujiza huu hayapokelewi vizuri na viongozi wa dini. Maandiko na Sheria vimegongana na upendo na ukarimu.

Unaweza kufikiria hiyo hali? Mwanamke aliyepinda anawekwa huru na anasimama wima. Mwanamke kutoka huko pembeni anapiga hatua na kuingia katikati ya sinagogi – naye anacheza!

Zungumza kuhusu usumbufu!

Kuwa mkarimu ni pamoja na kuona na kuwaita katikati wasiopendwa, walioharibika, wageni – wale walio ukingoni. Inahusu kuwafunika kwa kumbatio la joto la Mungu na kuzungumza maneno ya heshima, na ya thamani kwao. Ni hapa ambapo nguvu ya Mungu ya kubadilisha ya ukarimu inaonekana. Ni hapa ambapo uponyaji, ukamilifu na tumaini hutolewa.

Kwa ajili ya kutafakari:

Nani yuko pembeni, kwenye ukingo wa jamii yetu ya imani?

Nani anatuhitaji tumwone, tumwite aje mbele, tumjumuishe, tumkumbatie na tumheshimu?

Vipingamizi katika jamii yetu ya imani ni vipi vinavyozuia watu wasije kwake Yesu?

Maombi kwa siku ya leo:

Bwana, tupe macho ya kuona; moyo wa upendo wa kukumbatia na kuwajumuisha wengine; na ujasiri wa kutoa ukarimu...hata wakati ambao ukarimu husababisha usumbufu. Amina.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Fungua Milango. Fungua Mioyo.

Tukiwa na milango iliyofunguliwa na mioyo iliyofunguliwa, tunaweza kuwakaribisha wengine mahali watakapoonekana, wanapopendwa na pale wanapothaminiwa. Katika mfululizo huu wa siku nane, tunakualika uangalie kwa karibu mifano na hadithi za ukarimu zinazopatikana katika Biblia na uwe na muda wa kutafakari jinsi wewe unavyoweza kufanya ukarimu vizuri kwa kutumia maisha yako mwenyewe.

More

Tungependa kumshukuru Salvation Army kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://salvationarmy.org