Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 3 YA 31

Imani ndiyo iliyomsukuma Ibrahamu kuitii sauti ya Mungu na kumtoa sadaka Isaka, mwana wake wa pekee. Mungu ndiye aliyempatia Isaka, na Ibrahimu akiamini ahadi ya Mungu alitegemea kuwa Mungu ataweza kumfufua Isaka kutoka kwa wafu. Ndivyo ilivyotokea kimfano Mungu alipomrejeshea tena Isaka. Hivyo tendo la Ibrahimu lilipata kuwa ushuhuda kuhusu tendo la Mungu ambalo lilifanyika baadaye alipomtoa Mwanawe pekee kama sadaka ya dhambi na kumfufua tena kutoka kwa wafu. Mungu atukuzwe daima!

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz