Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Mababa wa imani kama vile Ibrahimu, Isaka na Yakobo walikuwa na uhusiano wa karibu na Mungu kupitia kuisikia na kuitii sauti ya Mungu kwa imani. Sara alipokea ahadi ya mtoto kwa kuamini kuwa Mungu ni mwaminifu na atatenda alichoahidi. Hao wote walidumu katika imani hadi kufa. Imani hiyo iliwafanya kuwa wageni wapitao hapa duniani na warithi wa nchi ya mbinguni. Sisi tuige mfano wao mzuri tukiisikia na kuitii sauti Mungu ili sisi nasi tuweze kufika mbinguni na kuurithi uzima wa milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz