Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Dhambi ni mzigo unaotulemea hata tukashindwa kusonga mbele katika safari yetu ya imani. Tunawezaje kutua mzigo huo? Hutokea tukimtazama Yesu Kristo. Alituanzishia imani, naye ataitimiza, akituvuta kwa upendo wake ili tusimame imara katika imani yetu. Kwa hiyo ni muhimu kulitafakari Neno la Mungu kila siku ili lituimarishe tusije tukalemewa na mambo ya dunia, yakatuchosha na kutupotosha. Habari ya Yesu kuketi kwa Mungu ituambie kuwa ameshinda yote. Tukimtazama Yeye, hatutapoteza imani yetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz