Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Machozi siyo ishara ya hakika ya toba. Mungu alimpa nafasi ya kutubu, ila Esau hakuiona, maana alitafuta tu kubarikiwa. Mfano wa Esau hutuonya. Kuna watu wanaosikia uchungu, Mungu asipowafanyia wanavyotazamia bali kuwarudi.Endeleeni kutembea katika njia iliyonyoka(m.13 BHN), tunahimizwa, tukikumbushwa mambo mawili: 1) Tukipokea adhabu ya Mungu, kunamatunda ya haki yenye amani(m.11). 2) Neema ya Mungu huleta motisha ya kustahimili. Kwa hiyo tunaambiwa kuangaliasana mtu asiipungukie neema ya Mungu. Kama neema haipo, kuna hatari yashina la uchungukuchipuka (m.15, lakini kama ipo, inamfanya muumini kutafutakwa bidii kuwa na amani na watu wotena kuishi maisha yautakatifu(m.14).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz