Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Yesu habadiliki wala neema ya Mungu. Hii ndiyo inayotuimarisha. Vitu vya nje kama vile kula nyama ya wanyama waliotolewa sadaka, havina faida. Katika agano la Sinai nyama ya dhabihu za dhambi haikuliwa bali iliteketezwa nje ya kambi. Hata hili Yesu amelitimiza alipokufa kifo cha laana nje ya Yerusalemu. Yeye akitutakasa tutakuwa huru kweli mbali na dhambi. Basi, tushikamane naye hata katika shutumu lake. Na tuige imani ya viongozi wetu waliotangulia kumfuata Yesu namna hiyo.Basi, kwa njia yake[Yesu], na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu(m.15-16).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz