Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 18 YA 31

Ni bahati kwetu kwamba Yesu mwenyewe ameufafanua mfano huu katika m.37-43:Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao.Mfano hausemi juu ya wana wa ufalme wa Mungu na wana wa yule mwovu kuishi pamoja ndani yakanisa. Kuhusu jambo hili Yesu ametoa mafundisho katika Mt 18:15-17 (ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru). Bali mfano katika somo la leo unasema juu ya wana wa ufalme na wana wa yule mwovu kuishi pamoja katikaulimwengu huu(m.38,lile konde niulimwengu). Kwa mfano huu Yesu anakataza tabia ya kutaka kuendeleza ufalme wa Mungu katika ulimwengu huu kwa kutumia nguvu na mamlaka ya kidunia.

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz