Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Mfano wa leo unahusu juya au nyavu iliyotupwa baharini. Mfano huu na mfano ule wa mbegu njema na magugu inasisitiza mambo mawili muhimu:1.Iko siku ambapo wanadamu wote, walio hai na wafu, watafika mbele ya Mwana wa Mungu.Atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi(m.40-41).Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki(m.49). Na kwa Yesu hakuna upendeleo. Atahukumu kwa haki kabisa, kwa sababu anajua yote.Hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu(Ebr 4:13).2.Yesu anasisitiza kwamba uzima wa milele upo, nawenye hakiwatakaoupatawataong'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao(m.43). Vilevile kifo cha milele kipo. Yesu anafafanua hali hiyokama tanuru ya moto, na watakaokwenda hapo niwatendao maasi.Ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno(m.40-42, 49-50). Anatuambia ukweli mtupu ili kutuonya, maana hapendi tupotee. Je, unaelekea wapi?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz