Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Mifano miwili midogo katika m.31-33 inahusu nguvu ya ajabu ya ufalme wa Mungu. Hili ni neno la kukutia moyo, wewe uliye mtumishi katika kanisa kwa namna moja au nyingine. Huenda wakati mwingine tunawaza kwamba wafuasi wa kweli wa Yesu ni wachache mno mahali tulipo sisi. Tena tunatambua upungufu wetu, na matunda ya kazi huonekana ni hafifu sana. Ndipo tunatarajia kukata tamaa. Hapo tunahitaji sana kuizingatia mifano hii miwili ya Yesu! Mifano miwili mingine katika m.44-46 inahusu uzuri wa ufalme wa Mungu. Yesu anasema kuwa mtu anayeuona ufalme huo yuko tayari kuuza vyote alivyo navyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz