Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 15 YA 31

Dunia ya leo ina tabaka la maskini na matajiri. Wapo wanyonge na wenye nguvu. Matajiri na wenye uwezo hawawakumbuki wanyonge, na badala yake wanawanyonya, wanaendelea kujilimbikizia mali bila kuwakumbuka maskini. Zaburi hii inawasa wenye navyo kuwasaidia wasio navyo na kuwatunza, kwani ndivyo Mungu atakavyowasaidia, hawa wenyewe wakipatwa na taabu na ugonjwa.Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.Bwana atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake umemtandikia(m.1-3). Swali la kujiuliza leo ni hili, Je, ni mara ngapi tunawajali maskini na wanyonge? Tafakari maana yake, Daudi akisema kwambaheri amkumbukaye mnyonge(m.1).

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz