Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Busara na hekima za kibinadamu haziwezi kutuokoa, bali kulitii Neno la Mungu kwa imani. Ndivyo ilivyo katika somo hili. Kama Jemedari Naamani na mfalme wa Shamu wangepuuza ushuhuda wa yule binti mtumwa wa Kiisraeli, basi shida ya Naamani isingekwisha. Na zaidi sana Naamani angepuuza neno la nabii Elisha kuhusu kuoga katika mto wa Yordani, basi ukoma wake ungebaki. Hata kama tukiona ni jambo dogo ambalo Mungu anatuambia, tulisipuuze Neno lake, bali tulifuata kwa utii wa imani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz