Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?(Rum 8:31). Washami walipopanga kupiga vita Waisraeli, Mungu alimjulisha mtumishi wake Elisha, naye akawajulisha Waisraeli. Mfalme wa Shamu alikasirika akidhani yupo msaliti katika jeshi lake. Hata alipotambua kuwa Elisha ndiye anayefichua siri, alituma jeshi kumkamata, lakini jeshi hilo lilitekwa na kutendewa mema kwa kufanyiwa sherehe, kisha kuachwa huru. Hapo Elisha alimshauri Mfalme kama Yesu anavyotuambia katika Mt 5:44, akisema,Mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. Kutokana na Mfalme kutowapiga Washami, amani ikatawala katika Israeli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz