Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Katika utangulizi wa waraka Paulo anajitambulisha wazi kuwa yeye yu nani. Ndiye Mtume wa Kristo Yesu. Kwa hiyo Timotheo apokee waraka wa Paulo kama neno la Mungu kwake. Paulo anamwona Timotheo kuwa mwana wake hasakatika imani.Ndivyo Paulo anavyoandika katika barua yake ya kwanza kwa Timotheo:Kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu(1 Tim 1:2). Imani hutupa kumwabudu Mungu kwa dhamiri safi katika hali zote, kama Paulo anavyoshuhudia katika m.3a akiandika:Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi.Pia tunatiana moyo kwa kushikamana na imani pasipo unafiki. Fikiri kidogo jinsi Paulo anavyosema imani ya familia ya Timotheo ilivyomsaidia: Natamani sana kukuona, ... nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo(m.4-5). Mimi na wewe tufuate mfano wa Paulo wa kuombeana kwa upendo na kutiana moyo katika huduma ya kueneza Injili.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz