Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

SIKU 6 YA 30

Tunaonywa dhidi ya ubishi wa maneno yasiyofaa. Maneno mara nyingi yamefarakanisha watu na kuleta mauvivu, mafarakano na ugomvi. Ni fundisho jema kwetu kuacha kulumbana katika maneno. Tunapaswa kujionyesha kuwa watendakazi wa Mungu kwa kusimamia neno lake la kweli. Ujumbe huu unafaa hasa kwa wakati wetu ambapo kuna mfumuko wa madhehebu. Mengi ya madhehebu haya ni matokeo ya maneno yasiyo na faida. TukumbukeMungu awajua walio wake. Hao ndio wamwitao Yesu kuwa ni Bwana na kuuacha uovu, kama ilivyoandikwa katika m.19:Msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz