Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Dalili za nyakati za mwisho zimeelezwa kuwa ni uasi kutawala, watu kujipenda wenyewe na kupenda fedha. Kuhusu dalili ya mwisho tunasoma katika 1 Tim 6:10 kwambashina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. Kiburi na uasi ndio huleta machafuko yote duniani, kwani ndani yake hakuna utii wala kumpenda Mungu. Je, tabia hizi zinapoenea, watu wa Mungu wafanye nini? Zingatia neno la 2:1 lina maana gani kwako:Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.Na fikiria vilevile Paulo anavyomkumbusha Timotheo katika 3:10-11:Wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso. Paulo anaendelea kuandika kwambaBwana aliniokoa katika hayo yote. Basi, tusikate tamaa, bali tujilinde na kulilinda Kanisa la Mungu kwa mafundisho ya neno la Mungu. Mungu ndiye awezaye kukomesha maasi yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz