Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Kusamehe na kutohukumu wengine ni mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe. Alitufundisha kuomba,Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu(Mt 6:12), na alituonya,Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi(Mt 7:1). Anapomaliza waraka wake, Mtume Paulo anawaombea wale wote waliomwacha alipojitetea kwa mara ya kwanza mahakamani. Anamwachia Mungu ahukumu juu yao na pia mpinzani Iskanda. Je, katika vikundi na makanisa ya waamini hakupo kukamiana na kuhukumiana? Mtume Paulo anatuonyesha tunaoamini mfano mzuri katika hayo na katika kumshukuru Mungu pamoja na kuishi kwa upendo wa kindugu miongoni mwetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz