Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Mungu hututaka tuwe wavumilivu hata mwisho, na Yesu anaahidi,Mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka(Mt 24:13). Eliya alipoanza safari yake ya mwisho, alimfanyia Elisha majaribio matatu ili amwache. Lakini Elisha alikataa kumwacha huku akimwapia kiapo cha kweli. Kwa kuambatana na Eliya hadi mwisho, Elisha alijitambulisha kama mtumishi mwaminifu, na Mungu aliweza kukubali ombi lake kuhususehemu marafufu ya rohoya Eliya (m.9). Maana ya ombi hili ni awe mrithi wa Eliya. Wale wote wenye kuvumilia hadi mwisho, hufurahia jibu zuri la Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz