Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Mungu ametuwekea mambo mawili: Baraka na laana. Naye hutusihi tuchague baraka ili tuwe na uzima:Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako(Kum 30:19). Miujiza ya kwanza ya Elisha ilikuwa ni mifano na alama za huduma mbili zilizomkabili. Huko Yeriko watu walipopata tabu ya maji yasiyofaa, aliyaletea uponyaji kwa jina la BWANA. Hii ni baraka. Katika mji wa Betheli vijana waliokosa adabu kwa nabii wa Mungu waliuawa kwa dubu. Hii ni laana. Huwaangukia watu wamkataao mjumbe wa Mungu. Tusimdharau BWANA wala yule aletaye ujumbe wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz