Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Ukengeufu katika imani ya kumwamini Mungu na kufuata miungu huleta shida kwetu wenyewe. Ahazi alikuwa hajatawala kipindi kirefu alipoanguka na kuumia. Alipaswa amtegemee Mungu wa kweli katika shida hii. Lakini yeye alituma wajumbe kuuliza kwa miungu ya kigeni kama angepona. Nabii Eliya aliwarudisha wajumbe kwa mfalme wakamwambie kuwa atakufa, kwa sababu hakumtegemea Mungu wa kweli. Kumwacha Mungu wa kweli na kutegemea miungu mingine au kitu kingine ni kukaribisha kufa.Kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi(Rum 8:13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz