Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

SIKU 3 YA 30

Paulo aliitwa kuwa Mtume wa Kristo ili aihubiri na kuifundisha Injili yake. Kwa kutii wito alioitiwa, Paulo amepatikana na mateso na kufungwa gerezani. Lakini haionei aibu Injili wala hamlaumu mtu yeyote kwa yaliyompata. Siri ya utulivu huu wa Paulo hata katika vifungo, mateso na dhiki ni nini? Anamjua Yesu! Naye ana uhakika kwamba kwa njia ya Roho Mtakatifu Yesu mwenyewe atamlinda pamoja na kile ambacho Yesu amempa. Hicho ndicho imani, upendo na tumaini kwa wokovu katika Yesu Kristo. Tafakari pia Paulo anavyosema katika Rum 5:3-5:Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz