Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Wana wa manabii walimwomba Elisha kwenda pamoja nao katika shughuli ya kupata miti ya ujenzi.Mmoja wao akamsema, ... nakusihi, uende pamoja na watumishi wako(m.3). Uwepo wake Nabii ulikuwa ni ishara ya kuwepo kwake Mungu pamoja nao. Haiwezekani kulieleza hili analolifanya Elisha bila kutaja nguvu na uweza alio nao Mungu. Mungu ndiye muumbaji. Ndiye aliyeweka nguvu ya uvutano ili vitu vianguke ardhini. Ndiye pia awezaye kufanya chuma kuelea. Mungu peke yake ndiye aliyeondoa dhiki ile, akijidhihirisha kwamba siku zote anaweza kuwategemeza. Sisi pia tumeahidiwa hivyo katika Zab 55:22:Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz