Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

SIKU 28 YA 30

Leo ni siku ya habari njema(m.9). Ni maneno ya wale wakoma ambao walitengwa kwa sheria za kidini ya Kiyahudi. Kama Wasamaria wakiwa na hali mbaya, bila shaka hali ya hao wanne ilikuwa mbaya zaidi. Kwa mtazamo wa kibinadamu, wazo lao halikuwa na tumaini, maana kwa Washami walikuwa adui wenye ugonjwa wa kuambukiza. Kumbe, Mungu huweza kutumia yeyote au chochote kuleta wokovu. Rudia m.9 ukiipima hali yako:Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.Je, wewe unayo habari njema? Unawashirikisha wengine au unatumia muda kwa mambo ya binafsi tu?

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2024

Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz