Soma Biblia Kila Siku 06/2024Mfano
Lengo la miujiza ni watu wapate kumwamini Mungu. Elisha alipokuwa katika chuo kimojawapo cha manabii kulikuwa na njaa kali, hata wakapaswa kula mboga na matunda ya mwituni. Mtu mmoja kwa bahati mbaya alichanganya mboga yenye sumu katika chakula. Kupitia Elisha, Mungu aliponya riziki ile kwa njia ya muujiza. Siku nyingine Mungu aliwalisha watu wake kwa mikate michache kama alivyofanya Yesu. Kuhusu hao waliolishwa na Yesu tunasoma katika Yn 6:14 kwambawalipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Watu wengine walipata kumwamini Yesu, wengine waliona mikate tu. Wewe umeona nini kutokana na somo la leo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa sita pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 2 Timotheo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz