Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Kukutana na Mungu kunabadilisha tabia na mwonekano wa mtu. Ndivyo ilivyotokea kwa Musa:Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling'aa kwa sababu amesema naye. Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling'aa; nao wakaogopa kumkaribia(m.29-30). Mabadiliko haya yanabeba ujumbe wenye sura ya Mungu wa utukufu. Kama ilivyoelezwa katika 2 Kor 5:17, mtu anayekutana na Kristo anakuwa kiumbe kipya:Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita; tazama! yamekuwa mapya.Pamoja na kumvaa Kristo, tunabadilika tufanane naye.Sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukirudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho(2 Kor 3:18). Watu waliuona uwepo wa Mungu usoni pa Musa. Vivyo hivyo Petro na Yohana walionyesha kwambawalikuwa pamoja na Yesu(Mdo 4:13). Sisi pia tunaweza kukaa naye kwa kuruhusu Neno la Mungu kukaa ndani yetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/