Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Mtumishi mwaminifu hataki kwenda peke yake, bali kuwa na uhakika kwamba Mungu ataongozana naye. Mungu ni nguzo ya maisha, wito na kazi yetu. Musa akimwomba Mungu anapata ahadi kwamba kwa sababu ya neema yake, Mungu hatamwacha. Ndipo Musa anaomba kuuona utukufu wa Mungu, lakini anaambiwa haiwezekani kwa mtu kumwona Mungu akaishi. Ila Musa anapata kuuona wema wa Mungu. Habari hii hutukumbusha Yn 1:18:Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua. Katika Kristo tunauona utukufu wa Mungu uliojaa neema. Kuzungumza na Kristo ni baraka.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/