Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano
Katika neema yake, Mungu anawaruhusu Waisraeli waendelee na safari yao, lakini dhambi yao imesababisha kwamba Mungu asiweze kwenda kati yao bila kuwaangamiza njiani. Wanaposikia habari hii ya hukumu wanalia. Wameelewa kuwa Mungu akimkataa mtu au taifa, matokeo yake ni maisha ya maumivu na majonzi. Kuna njia moja tu ya kuondokana na laana ya kukataliwa na Mungu. Ni kumrudia yeye kwa kutubu kweli, kama watu hao kutupa vyote vinavyohusiana na uovu wetu, na kusubiri Mungu atajibu nini. Tafakari ushuhuda wa Daudi katika Zab 32:4-5:Mchana na usiku mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi. Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka, Yoeli na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/