Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Ni Ijumaa Kuu. Asulubiwe! Hili ni itikio la Wayahudi walipoulizwa cha kumtenda Yesu asiyekuwa na makosa. Badala ya Yesu, walimchagua Baraba, mnyang’anyi (Yn 18:40, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi). Walipoulizwa tena, wakajibu, “Yesu asulubiwe.” Ni swali tunalopaswa kujiuliza hata leo, na hasa katika Juma Takatifu: Je, tunachagua nini badala ya Yesu? Mungu amemleta Yesu ili atukomboe sisi dhidi ya dhambi. Kumkosa yeye ni kukosa vyote, maana wote waliompokea aliwapa uweza wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (Yn 1:12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/