Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

SIKU 11 YA 30

Unaposikiliza mazungumzo ya wengi siku hizi, unagundua kuwa wanawasifu watu waliofanikiwa kupata mali nyingi. Sifa hizi hazizingatii mbinu anazotumia mtu anayesifiwa kupata mafanikio. Hata wapatao mafanikio ya mali kwa uhalifu wanaitwa wajanja. Neno la Mungu linaelelekeza vinginevyo: Usiwahusudu watu waovu, Wala usitamani kuwa pamoja nao; Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara (m.1-2). Mafanikio yadumuyo kweli ni yale yapatikanayo kwa kuifuata hekima ya Mungu. Neno la Mungu liwe kiongozi katika kufanya maamuzi yako. Pata ushauri kutoka hekima ya Yesu Kristo. Kwa ulitimia unabii katika Isa 11:2-3, Roho wa Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/