Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu (m.33). Yesu amewaeleza wazi yale yatakayotokea kwake (m.28-30). Kwa hiyo yatakapotokea, wataamini ya kuwa yeye ndiye. Wataona ushindi wake na watakuwa na amani ndani yake. Yesu ni Bwana wa amani (2 The 3:16). Ukimpokea yeye moyoni mwako utapata amani ya kweli aliyotuachia Bwana Yesu aliposema, Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo (Yn 14:27). Dhambi zako zimefutwa kwa damu yake!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/