Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Siku ya Mitende. Wayahudi walimtarajia mfalme atakayewaokoa dhidi ya utawala dhalimu wa Kirumi. Kwa hiyo wanauliza, Ni nani huyu (m.10)? Mshangao wao ulitokana na Yesu alivyoingia Yerusalemu atakapokamatwa na kufa msalabani. Watu walishangilia wakiimba, Hosana, yaani, Okoa sasa. Furaha hii inaonyesha utimilifu wa unabii unaosema, Tazama, mfalme wako anakuja kwako (Zek 9:9). Yesu akipanda punda ni alama ya upole, unyenyekevu na amani. Hivyo anaonyesha lengo lake kama mfalme ni kuwapa amani kwa Mungu (Rum 5:1, Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/