Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Ni Alhamisi ya Chakula cha Bwana. Ushirika Mtakatifu ni sehemu muhimu ya ibada ya Kikristo. Ni agizo la Yesu kuwa tukutanikapo katika Ushirika Mtakatifu, tufanye hivyo kwa ukumbusho wake: Akaumega mkate, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu (m.24-25). Inatukumbusha kifo cha Yesu msalabani ambapo alizichuka dhambi zetu. Kwa kupigwa kwake sisi tumepona (1 Pet 2:24; Isa 53:5). Lakini katika kushiriki tunatangaza pia kurudi kwake mara ya pili. Ndiyo maana tunaimba, Kufa kwake twakutangaza, kufufuka kwake twakukiri, kurudi kwake twakutazamia. Utukufu una wewe, Bwana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/