Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Kupatwa na majaribu katika maisha yetu ni jambo lisiloepukika. Jambo la msingi ni kuwa na imani kwa Mungu wetu awezaye kutuponya. Katika zaburi hii Daudi yuko katika hatari kubwa, naye anamwomba Mungu amwokoe. Hawa maadui ni maadui wa Mungu pia, watu wasiojali makuu aliyoyafanya. Daudi akiomba hivyo anatiwa uhakika kuwa Mungu atamjibu, na imani yake inaimarisha. Hivyo anataka hata wengine wapate kumfahamu Mungu kama Mlinzi na Mchungaji wao. Je, Bwana ni nguvu zako na ngome yako unayemkimbilia?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/