Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Ni sikukuu ya Pasaka. Msistaajabu, ... amefufuka; hayupo hapa ... enendeni mkawaambie (m.6-7). Maelekezo haya kwa wanawake walioenda kaburini kusitiri mwili wa Yesu, ni ujumbe wa matumaini. Walienda wakiwa na hofu, kwa sababu Bwana wao amekufa, na sasa ni siku ya tatu akiwa katika kaburi lililofungwa kwa jiwe kubwa. Kwa mshangao wanakuta kaburi wazi na kupokea ujumbe wa malaika kwamba Yesu hayupo kaburini, amefufuka. Tusikate tamaa wala kuogopa. Yesu amefufuka! Twendeni kutangaza habari hizi njema kwamba Yesu yu hai.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/