Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Mipango ya uovu huzaa mabaya. Matendo maovu ni matokeo ya mawazo yaliyo ndani yako mwenyewe, na yote ni dhambi (m.9a, Fikira za mpumbavu ni dhambi). Mawazo na matendo ni vema vipimwe na Roho Mtakatifu. Mungu anapenda maisha ya uadilifu. Tafakari mwenendo wako wa ndani ya moyo kabla ya kutenda chochote. Mwombe Mungu akusamehe dhambi ya kuwaza maovu. Moyo wako usivunjike kwa sababu ya majaribu yakupatayo. Usikubali hayo kuzaa dhambi, bali yakusogeze karibu na Mungu ili uimarike. Yakobo anashauri: Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili (Yak 4:7-8).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/