Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Mtu mwenye bidii ya kufanya kazi iliyo halali amejaa hekima. Kinyume chake, mtu mvivu hana akili. Je, akili uliyopewa na Mungu unaitumia namna gani katika kuleta mafanikio ya maisha yako? Tumia maarifa na ujuzi uliopewa na Mungu katika kugundua raslimali zinazokuzunguka. Jiepushe na hali ya uvivu, kwa faida ya siha, uchumi na akili yako. Bwana asema hivi, Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba (Yer 4:3). Omba akujalie hekima ya kuwa na moyo wa kutenda kazi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/