Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Wazazi wa Musa walioamua kumwasi Farao na kumficha mtoto wao ni wa kabila la Lawi. Waliposhindwa kumficha tena, walitengeneza kisafina cha manyasi, kilichopakwa lami ili kumhifadhi kando ya mto, huko wakimwacha Miriamu kumlinda. Mungu anamtumia binti Farao, ambaye anamhurumia mtoto aliyeachwa mtoni na kumwokoa. Binti Farao anamtafuta mwanamke wa kumnyonyesha kwa malipo na kuendelea kumlea mtoto kama wake mwenyewe. Hivyo bila kujua, binti Farao anatumikia mpango wa Mungu kuwaokoa watu wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/