Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Unafiki unaua mahusiano ya kweli. Upendeleo unaondoa utengemano na umoja wa jamaa, jamii na taifa. Atoaye haki afanye hivyo bila unafiki wala upendeleo. Mwanadamu hana haki kulipa kisasi. Hiyo ni kazi ya Mungu mwenyewe. Tena anasema, Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema (Rum 12:17-21). Tuifanye kazi kwa wakati unaotakiwa, tena unaofaa. Maamuzi ya kutenda chochote juu ya maisha na uhusiano na wengine yafuate kanuni bora ya Kristo katika Lk 6:31: Kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. Kumbuka amri ya Mungu inayosema, Usimshuhudie jirani yako uongo (Kut 20:16)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/