Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

SIKU 10 YA 30

Jumatatu ya Pasaka. Somo hili ni uthibitisho kwamba Kristo amefufuka. Alijifunua kwa wanafunzi wakiwa wamejificha, na sasa anajifunua kwa wafuasi wake wawili wakienda Emau. Kwa mashaka wanamwambia, Tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli – lakini sasa amekufa (m.21). Matumaini yao yameisha. Ila wanapoeleza mashaka yao kwa Yesu, yupo katikati yao. Akajifunua kwao. Matumaini yakarudi, nao wakarudi Yerusalemu kuwaeleza wenzao habari hizi. Tunaitwa kushuhudia habari njema za Yesu kwa watu wote.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/