Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

SIKU 5 YA 30

Si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao (m.20). Hao ni kwa mfano sisi Wakristo wa leo. Habari Njema ya Yesu Kristo imezidi kuenea katika dunia nzima kama Yesu alivyoagiza akisema nao, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari (Mt 28:18-20). Kama Yesu angaliwatoa Wakristo katika ulimwengu huu, Injili isingaliweza kuenezwa! Yesu hakuomba Mungu atutoe katika ulimwengu huu, kwa sababu kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni (m.18)! Yesu anakutuma!

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/