Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Uliyebatizwa na kumkubali Yesu kuwa Mwokozi wako, jua hakika kuwa Yesu Kristo anakuombea kwa Mungu Baba Mbinguni! Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea (Rum 8:34). Hutuombea nini? Somo la leo latupa jibu. Anatuombea ulinzi. Tutalindwa kwa kuliitia jina la Yesu Kristo. Mungu atulinde na nini? Atulinde na mafarakano. Yaani, Wakristo tuwe na umoja (m.11,Kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo). Pili atulinde na yule mwovu, yaani Shetani (m.15, Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu). Halafu anatuombea utakaso. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli (m.17).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/