Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Furahini siku zote;ombeni bila kukoma;shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu (m.16-18). Tukitaka kutimiza mapenzi hayo ya Mungu kwetu, tuanze na kumshukuru Mungu kwa vipaji vyake; tutashindwa kuacha kuomba, maana tutajaa furaha kwa ajili yao. Kama moto uzimikavyo, ukikosa hewa, Roho Mtakatifu hutuacha, akikosa mawasiliano kati yetu na Mungu, Mungu akiongea nasi katika Biblia, nasi tukiongea naye kwa maombi. Kwa hiyo twaonywa, Msimzimishe Roho (m.19). Unabii (m.20) si kutabiri mambo yajayo tu, lakini pia kuhubiri Neno la Mungu tukijua kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2 Pet 1:20f). Tusiudharau, bali tuupime na tuushike kwa imani unabii ule upatanao na Biblia. Hivyo twaepuka uovu kwa kujitenga na ubaya wa kila namna (m.22, Jitengeni na ubaya wa kila namna).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/