Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 1 YA 31

Mwaka wa 50 Paulo alifika Thesalonike, mji mkuu wa Makedonia, kwenye safari yake ya pili ya kueneza Injili, akakaa majuma 3 tu, akafukuzwa na Wayahudi, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako (Mdo 17:6). Hata hivyo usharika wa kudumu ulianzishwa. Sababu moja ya mafanikio hayo ni maombezi ya Paulo. Kwa mfano aliomba hivi, Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu (m.2). Tafakari alama za usharika hai kama zilivyoorodheswa katika m.3, Hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu. Yaani, tafakari 1. Imani itendayo, ikitegemea kazi ya wokovu iliyofanywa na Yesu. 2. Upendo udumuo kusaidia hata panapotokea taabu. 3. Tumaini katika kuja kwa Yesu liletalo faraja na kuwezesha kuangalia mbele kwa saburi.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/