Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Kwa sababu ya upendo wa Paulo kwa Wathesalonike, hakuweza kuvumilia (m.1 na 5) hali ya kutokuwa na habari yao. Kwa hiyo akamtuma Timotheo awaimarishe kiimani. Amani na maendeleo si uthibitisho kwamba tu Wakristo wa kweli. Dhiki za Kikristo ni tokeo la kuipokea Injili. Huja kwa sababu ya wasioamini (2:14, Ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi) na Shetani (m.5, Yule mjaribu akawajaribu), wala dhiki si alama ya kwamba hatumpendezi Mungu. Tukidhikiwa, twahitajiana. Ukiwa mlezi, uwafariji watoto wako wa imani kama Paulo alivyofanya alipomtuma Timotheo (m.2, Tukamtuma Timotheo ... ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu). Ukiwa mtoto kiimani, kusimama imara kwako humfariji mlezi wako kwa kuwa anajua taabu yake si bure (m.5, Nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/