Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Paulo anajitahidi kuomba awaone tena (3:10, Usiku na mchana tunaomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu), maana anaona ni Shetani anayemzuia (2:18, Tulitaka kuja kwenu ... mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia). Upendo ule ambao unamfanya Paulo awaombee ni kipaji cha Mungu kinachomiminwa na Roho mioyoni mwa watu wanapopata kuamini. Upendo ni kama tunda la imani linalokua na kujaa tele, hata muumini awe bubujiko la matendo ya upendo kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo (2 Pet 1:8). Pamoja na kuwafaidia wengine wote (m.12, Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote), kazi hiyo ya Mungu mioyoni mwa waumini huwaimarisha wenyewe wapate kusimama siku ya Bwana (m.13, Apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote). Matokeo ya maombi ya Paulo ni kuongezeka kwa imani ya waumini pamoja upendo wa mtu kwa mwenzake kuwa mwingi (2 The 1:3, Upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/