Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Bwana Yesu aja (3:13, Wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote)! Hivyo Wakristo waonywa waishi maisha maadilifu. Mungu hutaka waumini watakaswe (m.3, Haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu), kwa hiyo amewapa Roho Mtakatifu (m.8, Mungu anawapa ninyi Roho wake Mtakatifu). Maana ya "kutakaswa" ni maradufu: 1. Kutenganishwa na uovu (m.3 na 5-6, Haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati ... si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili). 2. Ili tumtumikie Mungu kwa miili yetu kama chombo (m.4, Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima). Hiyo ni kazi ya Mungu mwenyewe ndani yetu, kwa hiyo si maisha yetu maadilifu yanayotustahilisha siku ya hukumu. Lakini huyu asiyetaka kutakaswa bali kudumu katika dhambi, humkataa Mungu na kujiweka chini ya hukumu yake (m.8 na 6, Yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu. ... Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/