Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu (m.12). Wanaofanya hivyo usharikani kwa ajili ya waumini wenzao huonyesha wanavyowapenda. Walipiwe upendo kwa upendo, tukiwaheshimu kwa ajili ya kazi zao (m.13, Mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao). Angalia si kwa ajili ya cheo kile au heshima ile tu. Tafakari tofauti iliyo kubwa kati ya kawaida ya ulimwengu huu na upendo wa Yesu uliomiminwa mioyoni mwetu kwa njia ya imani: Wavivu hufukuzwa, sisi tuwaonye kwa upendo. Wanyonge hukanyangwa na kutumiwa vibaya, sisi tuwatie moyo na nguvu. Adui hulipiwa maovu kwa maovu, sisi tuwabariki na kuwaombea na kuwapenda kama tunavyoagizwa na Bwana Yesu: Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi (Mt 5:44).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/