Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Mariamu alionyesha upendo wake mkubwa kwa Yesu kwa kumpaka marhamu (manukato au uturi). Ni kitu kilichotoa harufu nzuri. Alimpaka kwa wingi, maana “ratli” ni sawa na nusu lita. Thamani yake ilikuwa kubwa sana (denari 300). Denari moja ilikuwa sawa na malipo ya kibarua ya siku moja! Pia alimpaka Yesu kichwani (ndivyo tunavyojifunza tukilinganisha na Mt 26:6-13). Leo twaweza kuonyesha upendo wetu kwa Yesu kwa kutoa mali au fedha zetu kwa kazi ya Injili, na pia kwa kuwasaidia wenye shida!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/